HOW KICD IS FLEECING PUBLISHING COMPANIES TO APPROVE BOOKS FOR CBC CURRICULUM

The write up below was done by a Swahili scholar who is privy to how the Kenya Institute of curriculum Development is minting billions from publishing firms in the name of approving their books for the new CBC CURRICULUM.

Sielewi.
Sijui mbona hadi sasa hivi mashirika ya uchapishaji humu nchini hayajadhihirisha wala kuonesha hasara au dhuluma yanazozipitia kwenye mchakato mzima wa uteuzi wa vitabu kule KICD!

Tangu uanzilishi wa mtalaa mpya wa umilisi (CBC) kwenye shule zetu, mashirika kupitia kwa waandishi wao yamekuwa yakichapisha vitabu na kuviwasilisha kwenye shirika la uundaji wa mitalaa (KICD) kwa kima cha shilingi elfu 60 kwa kila kitabu cha somo fulani ili kuhakikiwa na wahakiki maalum kabla ya kuidhinishwa na kuruhusiwa kutumiwa na wanafunzi wetu kwenye shule zetu! Kufikia sasa, yapo mashirika ambayo yamekuwa yakiwasilisha vitabu kwa kila mwaka na kwa bahati mbaya vitabu hivyo vikakosa kuidhinishwa kwa sababu za hapa na pale.

Hata hivyo, kwa tathmini na imani zangu ninakosa kuelewa ni vipi kitabu fulani kilichoandikwa na walimu wenye uzoefu na tajriba pana vikakosa kuidhinishwa kimfululizo kuanzia gredi ya 1 hadi 6 na hasa ikizingatiwa kwamba waandishi kwenye mashirika haya yote huviandika vitabu hivyo wakiongozwa na kudhibitiwa na mwongozo mmoja na unaofanana kwenye mashirika yote!

Hebu chukulia kuwa shirika limekuwa likiwasilisha mswada wa somo fulani kwa kima cha shilingi elfu 60 kwa kila kiwango au gredi, kufikia sasa shirika hilo litakuwa limeghirimika shilingi elfu 60 mara 6 (gredi ya 1 hadi 6), ambazo ni shilingi 360, 000. Na iwapo shirika limewasilisha miswada 6 kwa kila somo basi litakuwa limelipa shilingi 360,000×6 = 2,160,000. Na hizi hesabu ni kwa ajili ya vitabu vya mtalaa wa umilisi pekee (CBC)! Sijataja vile vya fasihi ambavyo pia hutozwa shilingi 140, 000 kwa kila kitabu kinachowasilishwa kule KICD kabla hata uhakiki na uidhinishwaji kuanza kufanywa! Kwa hivyo, iwapo shirika litakuwa limewasilisha vitabu 10 kwa mfano, shirika hilo litakuwa limelipa shilingi 140,000×10=1,140,000. Endapo vitabu vyote hivyo vikakosa kuidhinishwa, unaweza kukadiria hasara itakayolikumba shirika hilo! Wakadha, shirika lolote ambalo kitabu chake kimeidhinishwa, hulipa shilingi laki moja ili kukidhia harakati nzima ya uhakiki na uidhinishaji.

Idadi hiyo ya pesa kwangu naona ikiwa hasara, dhuluma, hujuma na ukatili mkubwa kwa mashirika yetu ya uchapishaji kwa vyovyote vile! Licha ya kiwango hicho cha pesa, zipo gharama nyingine za kuvichapisha vitabu hivyo kabla ya kuviwasilisha KICD, gharama za kuwalipia waandishi ada na milo za mikahawa wanapoishi wakati wa kuandika au kuvitunga vitabu hivyo.

Kwa maoni yangu, kutokana na hela hizo nyingi zinazotumiwa na mashirika ya uchapishaji kabla na wakati wa kuwasilisha miswada yao kwenye shirika la uundaji wa mitalaa (KICD), KICD ingeyahurumia mashirika hayo kwa kuidhinisha vitabu vyote vilivyowasilishwa kwa masharti fulani. Vilivyoidhinishwa viwe vya KIADA na vilivyosalia viwe vya ZIADA (baada ya masahihisho yaliyopendekezwa kufanywa).
Kigezo cha kuidhinisha mswada katika misingi ya bei yake na wala si ubora wake pia ni changamoto nyingine ambayo huenda ikawadumaza na kuwalemaza watoto wetu kielimu. Kwa maoni yangu, ubora wa kitabu ungalizingatiwa kuliko bei yake.

Vivyo hivyo, isisahaulike kuwa vitabu hivi ambavyo serikali inayashinikiza mashirika kuviuza kwa bei ya kiwango cha chini kabisa au kwa bei ya mchele kwenye gilasi, viliwanyima waandishi usingizi kwa muda wa siku kadhaa ndiposa wakaviandika! KUANDIKA SI RAHISI, NAOMBA NIRUDIE TENA KUWA KUANDIKA SI RAHISI! Kazi za waandishi zizifanyiwe mizaha kwa vyovyote vile licha ya sababu za hapa na pale!

Hatimaye, ningependa kusema kuwa, iwapo mchakato mzima wa uwasilishaji, uhakiki na uidhinishaji hautachunguzwa, kuangaziwa na kutathiminiwa kwa jicho la ndani na kwa haraka iwezekanavyo, huenda mustakabali wa vipaji vya waandishi chipukizi na wale tajika ukafishwa kwa lazima, mashirika chipukizi na yale tajika yakahofia kuwasilisha miswada yao kutokana na ada kubwa inayotozwa na shirika la uundaji wa mitalaa (KICD) na hatimaye miswada yao ikakosa kuidhinishwa. Vile vile, mwishoni mwa yote huenda wanafunzi wakamalizia kuidhinishiwa vitabu vibovu na visivyokidhi mafunzo toshelevu. Huku kutakuwa kumekidumaza na kukilemaza kabisa kizazi cha halafu.

NAHOFIA!

Published by MWALIMU Amunga Akhanyalabandu

Passionate about Advocacy on the REAWAKENING teachers in Kenya and reporting on the MULEMBE Nation. Having worked at the Kenya National Union OF TEACHERS in the advocacy department, I will be able to detail and explain about the welfare of teachers and their point of view on socio economic and political matters. Luhyia are the 2nd most populous ethnic group in Kenya. They are blessed with great land, topography, climate, resources and human Resource. We are also keen on Luhya Renaissance is about making the Mulembe People aware of their blessings, appreciating those blessings, defending them and putting them to proper use for the current and future generations.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s